Mafunzo

KOZI ZINGINE TUNAZOFUNDISHA 

1.Udereva wa magari ya shule.                                    

2. Kozi ya alama na sheria kwa madereva wote

MAFUNZO YANAYOTOLEWA NA CHUO.  

MAFUNZO YA UDEREVA YA MWEZI MMOJA/ ONE MONTH COURSE: Hili ni darasa la kila siku ambalo mwanafunzi huripoti kila siku kwenye vituo vyetu/ofisi kati ya saa 1:30 asubuhi hadi saa 11:30 jioni kwa siku za kazi Jumatatu  hadi Ijumaa na jumamosi ni darasa la nadharia linaloanza (saa 2:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana ) muda wa kuendesha umekadiriwa kama nusu saa (dk 30).

MAFUNZO YA UDEREVA YA WIKI MBILI/ TWO WEEKS COURSE: Hili darasa linalomuhusu mtu mwenye muda mchache kwa kujifunza udereva na hawezi kupata mwezi mzima na hajui kabisa kuendesha gari mtu huyu atatakiwa kuhudhuria vipindi viwili kila siku ili kutimiza vipindi 20 vya mwezi mzima ndani ya wiki mbili.

MAFUNZO YA UDEREVA YA WIKI MOJA TU (INTENSIVE/CLASH PROGRAM). Hili ni darasa linalochukua muda wa siku saba  (7) tu. Kwa mwanafunzi kuwa dereva bora, katika darasa hili mwanafunzi anatakiwa kuwa na muda usiopungua masaa matatu (3). Kwa siku na akili yake iwe imetulia kabisa. Atafanya mazoezi mengi na safari ndefu na baada ya siku 7 atakuwa amefuzu kabisa.

MAFUNZO YA UDEREVA KWA MFUMO WA DARASA LINALO  TEMBEA / MOBILE CLASS: Hili darasa linahusu mwanafunzi na mwalimu wake. Na gari ni la mwanafunzi. Ambapo mwalimu atamfundisha mwanafunzi kutoka nyumbani hadi eneo la kazi na kumrudisha hadi nyumbani kwake.

MAFUNZO YA FORKOLIFT
Mafunzo haya ni ya mwezi mmoja. Ambapo mwanafunzi atafundishwa namna ya kuopereti mashine na jinsi ya kufanya sevisi ndogondogo.

MAFUNZO YA NADHALIA.
Mafunzo haya yanamuhusu dereva aliyejifundisha mtaani au zamani hakumbuki mbinu bora za fani ya  udereva na hajui sheria na kanuni za usalama barabarani ikiwemo  udereva wa kujihami.

MAFUNZO YA UDEREVA WA  PIKIPIKI AU BAJAJI.
Kozi hii inachukua  wiki mbili mafunzo haya yanahusisha udereva wa bajaji au pikipiki


Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA FORKOLIFT