Maelekezo Muhimu
Utajiunga na mafunzo ya udereva kwa mujibu wa sheria ya usalama Barabarani ya mwaka 1973 ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania. Utapaswa kuhudhuria mafunzo siku zote kama itakavyoelekezwa.
Mafunzo yataendeshwa kwa muda wa mwezi mmoja (1) hiyo itakuwa kwa siku za kazi tu yaani Jumatatu hadi Ijumaa ni mafunzo ya vitendo kwa muda wa dakika 30 kwa kila mwanafunzi.
Siku ya Jumamosi ni mafunzo ya nadharia (Darasani) kuanzia saa mbili (2:00) asubuhi hadi (6:00) saa sita mchana.
Wanafunzi wote walioandikishwa katika ofisi mbalilmbali darasa litafanyika shule ya msingi Kibasila. Mahali shule ilipo panda magari yanayopita barabara ya Mandela au chang’ombe shuka kituo cha Serengeti. Utaona sehemu ya bustani ya maua ndani ya ukuta ndio shule ya Msingi iliko.
Shule ndio itakayoshughulikia upatikanaji wa Leseni ikisaidiana na mwanafunzi.Walimu wote wanaotoa mafunzo, wanauzoefu na mbinu mbalimbali kwa wanafunzi waoga kuwafanya wawe na ujasiri wa kutembeza gari barabara zote za hapa DSM.
Comments
Post a Comment